Kwa mujibu wa shirika la habari "Abna" kwa kunukuu "Al-Mayadeen", Upinzani wa Kiislamu wa Lebanon Hizbullah ulitoa taarifa yenye maneno makali kujibu hatua hiyo ya uadui ya Wizara ya Hazina ya Marekani ya kuweka vikwazo vipya dhidi ya harakati hiyo.
Katika taarifa ya Hizbullah imesemwa: "Madai ya serikali ya Marekani kwamba Hizbullah iko chini ya udhibiti wa Kikosi cha Quds cha Sepah-e Pasdaran wa Iran, ni kisingizio cha kuweka tena Hizbullah kwenye orodha ya vikwazo. Hatua hii ni sehemu ya sera za jumla za tawala za Marekani za kulenga, kuizingira na kushinikiza upinzani, mazingira yake ya kijamii na wafuasi wake."
Hizbullah iliongeza: "Vikwazo vipya vya Marekani vimewekwa kwa lengo la kulinda usalama wa adui, kuimarisha uvamizi kusini mwa Lebanon na kufungua njia kwa ajili ya kutekeleza miradi yake ya upanuzi. Hatua hii inathibitisha kwamba serikali ya Marekani, ambayo imezoea kutumia vikwazo kulazimisha utawala wake, bado inaendelea kushughulika na Lebanon kutoka nafasi ya ulezi. Serikali ya Marekani inajaribu kuwazingira Walebanon, kunyima Lebanon vyanzo vyake vya nguvu na kujaribu kuunda machafuko ya ndani."
Maoni yako